WANYONGE WASINYONGWE
WANYONGE WASINYONGWE
Wanyonge Wasijinyonge Wanyonge Wasinyongwe ni mkusanyo wa hatuba mbili zilizotolewa mjini Bukoba Februari 19, 2004 na Januari 31, 2017 na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Ndugu Pius B. Ngeze. Alikuw…
About This Content
Wanyonge Wasijinyonge Wanyonge Wasinyongwe ni mkusanyo wa hatuba mbili zilizotolewa mjini Bukoba Februari 19, 2004 na Januari 31, 2017 na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Ndugu Pius B. Ngeze. Alikuwa akiwatetea waendesha baiskeli na pikipiki wa mjini Bukoba kwa kuiomba serikali irekebishe sheria inayokataza vyombo vyenye magurudumu mawili kubeba abiria na kuwatoza nauli ingawa sheria hiyo inahusu vyombo hivyo kubeba abiria mradi bila kuwatoza nauli! Zimo pia makala zilizochapishwa na baadhi ya magazeti kuhusiana na hotuba hizo. Ndugu Ngeze kama Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa alikuwa akikisemea Chama katika mkoa wake, hususan, Chama Cha Mapinduzi katika Wilaya ya Bukoba Mjini, ambapo matawi yote 32, kata 13 kati ya 14 na kamati ya siasa ya wilaya waliishaamua hivyo. Mwenyekiti wa chama ndiye msemaji mkuu wa chama katika eneo lake. Hotuba zote mbili na, hasa ile ya pili, zilipokelewa kwa hisia tofauti. Waendesha pikipiki na baiskeli na watumiaji wa huduma hiyo nchi nzima walimpongeza. Watu wengine walimwona kama anatetea uvunjaji wa sheria. Ndugu Ngeze amekataa tafsiri hiyo ila amekuwa akiwatahadharisha viongozi wasome alama za nyakati. Hoja yake ni kuwatetea wanyonge wanaojaribu kujitafutia riziki, mtaji ukiwa ni nguvu zao. Anauliza sheria ipo kwa faida ya nani? Sheria gani haiwezi kurekebishwa? Hivi sheria inaweza kurekebishwa au kubadilishwa bila kulalamikiwa? Ni viongozi wangapi, hasa wa kisiasa wanaopingiwa kura, ambao hawaoni umuhimu na unyeti wa suala hili linalogusa wanyonge ambao ndiyo wengi wanapiga kura?
Publication Details
| Categories | Siasa, Uongozi |
| Publisher | TEPU |
| ISBN | 978-9987-07-001-4 |
| Publication Year | 2008 |
| Pages | 45 |
| Chapters | 11 |
| Language | Swahili |
| Keywords | WANYONGE |
| Academic | No |
| Visibility | Public |
| Formats |
Reading Access
Purchase or subscribe to unlock this content.
Open Reader