ELM-DIGITAL LIBRARY
Book

VITA KATI YA TANZANIA NA MAJESHI YA IDI AMIN YA KUKOMBOA KAGERA NA WAGANDA

by Johnstone R. Mujungu
Book Purchase + Subscription 3000 TZS
VITA KATI YA TANZANIA NA MAJESHI  YA IDI AMIN YA KUKOMBOA KAGERA  NA WAGANDA
Type Book
Access Purchase + Subscription
Language Swahili
Published Aug 14, 2026

VITA KATI YA TANZANIA NA MAJESHI YA IDI AMIN YA KUKOMBOA KAGERA NA WAGANDA

by Johnstone R. Mujungu
Book Purchase + Subscription 3000 TZS

Jenerali Idi Amin, alipompindua Rais Milton Apolo Obote, 25 Januari, 1971, Waganda, hasa, Baganda wa Ufalme wa Buganda, walifurahia mapinduzi hayo, kutokana na kuwa Obote alikuwa amemwondoa madarakani Mfalme wao, Ra…

About This Content

Jenerali Idi Amin, alipompindua Rais Milton Apolo Obote, 25 Januari, 1971, Waganda, hasa, Baganda wa Ufalme wa Buganda, walifurahia mapinduzi hayo, kutokana na kuwa Obote alikuwa amemwondoa madarakani Mfalme wao, Rais Kabaka Edward Mutesa na kwenda kuishi uhamishoni Uingereza mwaka 1966. Alifia huko 1969. Aidha, Amin aliwafukuza wafanyabiashara wenye asili ya Asia na kuwakabidhi biashara zao maafisa wa Jeshi lake na baadhi ya Waganda, kitendo ambacho walikifurahia. Lakini, furaha yao haikudumu kwa muda mrefu. Idi Amin alipogundua harakati zilizokuwa zinaendeshwa nje na ndani ya nchi yake, ya waliotaka kumuondoa madarakani, hasa, Milton Apolo Obote, wafuasi wake na vikundi vingine, alianza kuua watu wote aliowashuku kuwa na uhusiano naye na wanaharakati wengine. Kama utakavyoona katika sura ya 3, viongozi wa kisiasa, kijeshi na kidini wa zamani waliosalia nchini Uganda na hata waliokuwa katika serikali yake (Amin) waliuawa. Waliouawa ni pamoja na Mawaziri, Mabalozi, Viongozi wa kijeshi (jeshi la nchi, polisi, magereza, usalama wa taifa n.k.), Viongozi wa kidini, wakiwamo Maaskofu, Maofisa watendaji wakuu wa serikali, wanaharakati, Wafanyabiashara wakubwa, wakati na watu mashuhuri katika jamii wa makabila yote, hasa, wa kabila ya Obote, wafuasi wa Chama cha Siasa cha Obote, UPC n.k. Watu wengi waliuawa baada ya kuteswa sana, kuburuzwa katika barabara za Kampala, kupotea na kutupwa katika Ziwa Victoria na mito, hasa, Mto Nile. Watu wengi waliouawa hawakujulikana walikozikwa wala kujulikana mwisho wa maisha yao ulikuwaje. Inaaminika, hakuna familia ya Uganda (ukiondoa kabila la Amin) ambayo haikufiwa na mwanafamilia au mwanaukoo. Kwa hakika watu walimchukia sana mtu waliyemshangilia mwanzoni, lakini, hawakuwa na namna ya kumaliza utawala wake. Kutokana hali hiyo, Waganda waliishi kwa hofu na wasiwasi mkubwa. Walimwomba sana Mwenyezi Mungu amalize mateso na majonzi yao.

Publication Details

Category VITA NA AMANI
Publisher TEPU
ISBN 978-9976-58-426-4
Date Published 2026-08-25
Publication Year 2022
Pages 281
Chapters 27
Language Swahili
Keywords Historia ya vita ya Kagera
Academic No
Visibility Public
Formats PDF

Reading Access

Purchase or subscribe to unlock this content.

Open Reader

Share & engage

No ratings yet — be the first.
Your rating
Comments

No comments yet.

Report this content