ELM-DIGITAL LIBRARY
Book

RAIS SAMIA NA MAGEUZI YA SEKTA YA BIASHARA TANZANIA

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 3000 TZS
RAIS SAMIA NA MAGEUZI YA SEKTA  YA BIASHARA TANZANIA
Type Book
Access Purchase + Subscription
Language Swahili
Published Aug 14, 2026

RAIS SAMIA NA MAGEUZI YA SEKTA YA BIASHARA TANZANIA

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 3000 TZS

Rais Samia Na Mageuzi Ya Sekta Ya Biashara Tanzania Sekta ya biashara ni mhimili muhimu wa maendeleo ya taifa lolote. Kupitia biashara, nchi hujenga uchumi wake, kuongeza pato la taifa, kufanikisha ajira, kukuza sekta…

About This Content

Rais Samia Na Mageuzi Ya Sekta Ya Biashara Tanzania Sekta ya biashara ni mhimili muhimu wa maendeleo ya taifa lolote. Kupitia biashara, nchi hujenga uchumi wake, kuongeza pato la taifa, kufanikisha ajira, kukuza sekta binafsi na kushirikiana na mataifa mengine katika misingi ya usawa wa kiuchumi na kijamii. Tanzania, tangu enzi za kabla na baada ya Uhuru, imepitia mageuzi mbalimbali ya kibiashara kulingana na mazingira ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyokuwepo. Mageuzi hayo yameacha alama katika maisha ya Watanzania, lakini pia yameibua changamoto ambazo zilihitaji majibu ya kisera na kiuongozi. Katika mazingira haya, uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umejitokeza kama kipindi cha mageuzi makubwa yenye mwelekeo wa kisasa na kimkakati katika sekta ya biashara Tanzania. Tangu aingie madarakani mwaka 2021, Rais Samia ameweka msisitizo wa pekee kwenye diplomasia ya uchumi, uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji, kuondoa urasimu, kuimarisha ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma, pamoja na kufungua milango ya biashara za kimataifa kwa uwazi na mashirikiano mapya. Hatua hizi zimeashiria Tanzania mpya inayojiandaa kushindana kikamilifu katika soko la kikanda na la kimataifa. Kitabu hiki kimeandikwa ili: 1. Kueleza historia na change 2. moto za sekta ya biashara kabla ya kipindi cha Rais Samia, 3. Kuchambua mageuzi ya kisheria, kisera na kitaasisi yaliyotekelezwa chini ya uongozi wake, 4. Kufafanua mchango wa mageuzi hayo kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa, 5. Kuchambua nafasi ya Tanzania katika biashara za kimataifa, 6. Kutathmini mafanikio, changamoto zinazobakia na mustakabali wa mageuzi ya kibiashara. Ni matumaini ya mwandishi kwamba wasomaji wa kitabu hiki—wakiwemo wafanyabiashara, wanasiasa, wanazuoni, wanafunzi, watunga sera, viongozi wa vyombo vya kifedha na wananchi kwa ujumla—wataona mchango mkubwa wa mageuzi haya katika kufungua fursa za biashara, kuongeza ushiriki wa wananchi katika uchumi, na kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye ushindani wa kweli katika biashara za kikanda na kimataifa. Aidha, kitabu hiki kinatoa tafsiri ya kisayansi na kivitendo ya mageuzi yanayoendelea chini ya Rais Samia. Kwa mantiki hiyo, kitakuwa rejea kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, rejea kwa watunga sera na viongozi wa serikali, na mwongozo wa kivitendo kwa wafanyabiashara na wawekezaji ndani na nje ya Tanzania. Mwandishi anaamini kuwa mageuzi ya kibiashara siyo safari ya mtu mmoja bali ni safari ya pamoja. Rais Samia ametoa dira na msukumo, lakini utekelezaji wake unahitaji mshikamo wa sekta binafsi, sekta ya umma, taasisi za kifedha, vyuo vya elimu, pamoja na wananchi kwa jumla. Kwa kushirikiana, Tanzania inaweza kufikia uchumi shindani, wa kisasa na unaoleta ustawi wa wengi. Kwa roho ya mshikamano wa kitaifa, mshikamano wa kikanda, na mshikamano wa kidunia, basi tuingie pamoja katika safari hii ya kimaandishi ya kuchunguza na kujifunza kuhusu “Rais Samia na Mageuzi katika Sekta ya Biashara Tanzania.”

Publication Details

Category MCHANGO WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Publisher TEPU
ISBN 978-9976-58-488-2
Publication Year 2025
Pages 131
Chapters 35
Language Swahili
Academic No
Visibility Public
Formats PDF

Reading Access

Purchase or subscribe to unlock this content.

Open Reader

Share & engage

No ratings yet — be the first.
Your rating
Comments

No comments yet.

Report this content