MCHERA ZIWANI
MCHERA ZIWANI
Mchera Ziwani ni hadithi inayohusu Mzee Wimbi na mwanae Mchera, mke wa Mchera, Mishosho na mrembo aitwaye Kanyindo. Mwanzoni Mchera alikuwa mchongaji wa vinyago na baba yake Mzee Wimbi, alikuwa mvuvi. Baada ya kupung…
About This Content
Mchera Ziwani ni hadithi inayohusu Mzee Wimbi na mwanae Mchera, mke wa Mchera, Mishosho na mrembo aitwaye Kanyindo. Mwanzoni Mchera alikuwa mchongaji wa vinyago na baba yake Mzee Wimbi, alikuwa mvuvi. Baada ya kupungua kwa miti inayofaa kuchongwa vinyago, Mchera aliamua kujifunza uvuvi, kutoka kwa baba yake. Hata hivyo, Mzee Wimbi alimtahadharisha Mchera kuwa wakati wote asiende kuvua samaki katika eneo la ziwa la watu waitwao Walaghai. Mchera alikubaliana naye. Baada ya samaki kupungua katika eneo lao la ziwa, ili aendeleze mapato yake, Mchera aliamua kwenda kutega samaki katika eneo la Walaghai. Alipokuwa katika shughuli hiyo, ghafla Mchera alimwona mrembo aliyeitwa Kanyindo. Alimpenda na kumwomba amwoe. Lakini, kabla hajakubali, Kanyindo alimtaka Mchera amletee kwanza mkufu wa mke wake, aliopewa na wazazi wake kabla ya kuolewa. Ili kupata mkufu huo, Mchera alirudi nyumbani usiku na kumvamia mke wake wakati amelala, alimnyang’anya mkufu huo. Mkewe alipiga kelele za “Mwizi! Mwizi!” Mchera alifanikiwa kuiba na kumpelekea Kanyindo. Je, Kanyindo aliupokea mkufu huo na kukubali kuolewa na Mchera? Mke wa Mchera alichukua hatua gani? Mwisho wa ndoa ya Mchera na Mishosho ni upi? Majibu yako kitabuni.
Publication Details
| Category | Riwaya |
| Publisher | TEPU |
| ISBN | 978-9987-88-331-8 |
| Date Published | 2022-06-30 |
| Publication Year | 2022 |
| Pages | 60 |
| Chapters | 5 |
| Language | Swahili |
| Keywords | Hadithi, Riwaya |
| Academic | Yes |
| Visibility | Public |
| Formats |
Reading Access
Purchase or subscribe to unlock this content.
Open Reader