MAJIGAMBO YA WADUDU
MAJIGAMBO YA WADUDU
Majigambo ya Wadudu ni kitabu kinachoeleza sifa na tabia za wadudu. Wadudu walikutana kwa lengo la kufahamiana na kumchagua Kiongozi wao. Mkutano wa uchaguzi uliendeshwa na Panzi kama Mwenyekiti. Wadudu waliohudhuria ni…
About This Content
Majigambo ya Wadudu ni kitabu kinachoeleza sifa na tabia za wadudu. Wadudu walikutana kwa lengo la kufahamiana na kumchagua Kiongozi wao. Mkutano wa uchaguzi uliendeshwa na Panzi kama Mwenyekiti. Wadudu waliohudhuria ni Mende, Inzi, Kipepeo, Mbu, Nyuki, Mbung’o, Konokono, Nge, Jongoo, Sisimizi na Funza. Kila mdudu alieleza sifa zake mbele ya wenzake ili aweze kuchaguliwa kuwa Kiongozi wao. Michoro ya wadudu hao iliyomo kitabuni ni ya rangi na kwa hakika watoto wataipenda. Aidha, watoto watajifunza jinsi wadudu hao walivyo, sifa na tabia zao ili waweze kujikinga na madhara wanayoyasababisha kwa binadamu. Ni kitabu kizuri kwa watoto.
Publication Details
| Categories | HADITHI FUPI ZA WATOTO NA VIJANA, VITABU VYA WATOTO VYENYE MICHORO |
| Publisher | TEPU |
| ISBN | 978-9987-67-108-3 |
| Date Published | 2013-05-06 |
| Publication Year | 2013 |
| Pages | 16 |
| Chapters | 1 |
| Language | Swahili |
| Keywords | kids |
| Academic | Yes |
| Visibility | Public |
| Formats |
Reading Access
Purchase or subscribe to unlock this content.
Open Reader