Kilimobiashara na Kanuni ya Kukifanikisha
Kilimobiashara na Kanuni ya Kukifanikisha
Kilimobiashara kinahusu kilimo na shughuli zote zinazohusika na kilimo kuanzia uzalishaji, utayarishaji, usindikaji, usambaji, usafirishaji, utengenezaji wa zana za kilimo, uuzaji n.k. Kilimobiashara ni kilimo cha ngaz…
About This Content
Kilimobiashara kinahusu kilimo na shughuli zote zinazohusika na kilimo kuanzia uzalishaji, utayarishaji, usindikaji, usambaji, usafirishaji, utengenezaji wa zana za kilimo, uuzaji n.k. Kilimobiashara ni kilimo cha ngazi ya juu ambacho ni kinyume cha Kilimo cha Mazoea au Kilimo cha Kujikimu. Ni kilimo kinachoendeshwa kitalaamu na kibiashara, kikizingatia kanuni za biashara na utalaamu. Lengo lake ni kupata mavuno mengi au makubwa (ya mimea ya mazao, mifugo, miti, malisho n.k.) na yaliyo na ubora wa hali ya juu, kwa ajili ya soko. Matokeo yake ni kupata mapato makubwa baada ya kuuza kutoka eneo dogo la ardhi na kumzidi mkulima anayetumia eneo kubwa la ardhi bila kuzingatia kanuni za kilimobiashara. Lengo kuu la kilimobiashara ni kupata faida kubwa ndani ya muda mfupi inavyowezekana baada ya kuuza. Kilimobiashara ni kilimo cha soko. Bila kuwa na hakika ya wateja wa kununua mazao yako, usiwekeze katika kilimobiashara cha aina yoyote. Utafiti wa soko la muda mrefu, muda wa kati au endelefu ni muhimu kabla ya kuanzisha kilimobiashara cha aina yoyote. Uwekezaji katika Kilimobiashara ni moja kati ya Miradi ya Kibiashara ambayo mwekezaji yeyote anaweza kuchagua. Kilimobiashara kinaweza kuwa shamba dogo au shamba kubwa la mimea ya mazao, mifugo midogo na mikubwa, samaki, nyuki n.k. Ni aina ya kilimo kinachohitaji Mtaji, Usimamizi makini na wa karibu wa mwekezaji mwenyewe, Utalaam wa kisasa, ubunifu, menejimenti makini na inayojua na matumizi ya watalaam wa aina kadhaa katika uzalishaji, uuzaji, ufungashaji, upangaji madaraja wa mazao, hifadhi, usafirishaji n.k. Hiki ni kitabu cha lazima kwa yeyote anayetaka kuwekeza katika Kilimobiashara cha aina yoyote.
Publication Details
| Category | Agriculture |
| Publisher | TEPU |
| ISBN | 978-9987-58-421-9 |
| Date Published | 2026-08-10 |
| Publication Year | 2024 |
| Pages | 40 |
| Chapters | 6 |
| Language | Swahili |
| Academic | No |
| Visibility | Public |
| Formats |
Reading Access
Purchase or subscribe to unlock this content.
Open Reader