ELM-DIGITAL LIBRARY
Book

KILIMO BORA CHA MIHOGO

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 2000 TZS
KILIMO BORA CHA MIHOGO
Type Book
Access Purchase + Subscription
Language Swahili
Published Aug 08, 2026

KILIMO BORA CHA MIHOGO

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 2000 TZS

Muhogo ni moja ya mazao ya mizizi ambayo ni muhimu sana kwa chakula nchini. Umuhimu wake unatokana na uwezo wake wa kustawi na kutoa mavuno ya kuridhisha katika mazingira ya ukame na udongo usiokuwa na rutuba nyingi …

About This Content

Muhogo ni moja ya mazao ya mizizi ambayo ni muhimu sana kwa chakula nchini. Umuhimu wake unatokana na uwezo wake wa kustawi na kutoa mavuno ya kuridhisha katika mazingira ya ukame na udongo usiokuwa na rutuba nyingi ambapo mazao mengine yasingeweza kustawi. Hustawi katika sehemu nyingi, hasa, za ukanda wa chini na miinuko ya kadiri.Aidha, ni chakula kikuu cha zaidi ya watu milioni 300 duniani na mamilioni ya mifugo. Wanga unaotokana na zao hili una matumizi mengi. Kuna viwanda vingi duniani ambavyo hutumia muhogo kutengeneza bidhaa mbalimbali. Viwanda hivyo huajiri maelfu ya watu. Kwa upande mwingine, huko nyuma zao hili lilijulikana kama zao la watu fukara na halikufanyiwa utafiti wa kutosha. Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni wataalamu wamegundua mambo matatu muhimu sana kuhusiana na zao hili: kwanza, ukiondoa miwa, ni zao pekee linalotoa wanga mwingi zaidi kutoka hekta (au sehemu yake) moja ya ardhi kuliko zao lingine. Pili, ni zao linalovumilia ukame. Tatu, lina wadudu na magonjwa machache ukilinganisha na mazao ya nafaka. Kwa mfano, mimea ya muhogo haishambuliwi na nzige. Kwa hiyo, kama balaa la nzige likitokea, wakulima wataponea kwenye mashamba ya muhogo wakati mazao mengine yatakuwa yameteketezwa na wadudu hao.

Publication Details

Category Kilimo
Publisher TEPU
ISBN 978-9987-67-151-9
Date Published 2026-08-07
Publication Year 2023
Pages 108
Chapters 16
Language Swahili
Keywords MIHOGO
Academic Yes
Visibility Public
Formats PDF

Reading Access

Purchase or subscribe to unlock this content.

Open Reader

Share & engage

No ratings yet — be the first.
Your rating
Comments

No comments yet.

Report this content