JASUSI ALIYEMUUA BOSI WAKE
JASUSI ALIYEMUUA BOSI WAKE
Katika hila zao za kutetea haki za wanawake, utadhani si haki za binadamu, wanaharakati wa Kimagharibi wanajikuta wakimtwisha mwanamke wa Kiafrika mzigo mzito wa kusaka noti kama baba, juu ya mzigo wa kimi…
About This Content
Katika hila zao za kutetea haki za wanawake, utadhani si haki za binadamu, wanaharakati wa Kimagharibi wanajikuta wakimtwisha mwanamke wa Kiafrika mzigo mzito wa kusaka noti kama baba, juu ya mzigo wa kimila wa kulea watoto na kutunzbe walikuwa na ajenda ya siri ya kuzibomoa familia imara za Kiafrika kwa lengo la kurudisha ukoloni. Lakini, wanagusa pabaya pale wanapomnasa mke wa Julio na kumjaza ujinga wa kutelekeza familia ili kuhamia mitaani kwa kisingizio cha kufanya ujasiriamali; wakimrubuni kwa vijisenti vya mikopo ya kuwakomboa wanawake kutoka kwenye mamlaka ya waume zao, au mfumo dume, kama wanavyouita! Na hicho ndicho kilichowaponza wahalifu waliojipatia mamilioni ya fedha kwa kuendesha shirika binafsi la kijasusi likitumia TEHAMA na maafisa wastaafu wa jeshi la polsi na jeshi la wananchi kuwanasa wake za watu waliowasaliti na kuwachukua video za matusi yao. Katika sakata la Julio kumkomboa mke wake, majasusi hawa pamoja na washirika wao wanajikuta wakipukutika kama kumbikumbi walipojaribu kutoroka kutoka kwenye pango la jumba lao la kifahari lililopo katikati ya msitu wa majanga wa Mabwepande, Dar es Salaam, Tanzania. Kila aliyechomoka alikutana na mtutu kabambe wa bastola ya mdunguaji sugu wa kike, Zuhura, au Kimbunga Katalina kwa rakabu yake. Ili kufahamu kiundani yaliyojiri msituni humo, katika pambano la Julio kumkomboa mke wake; na kupelekea kukomeshwa kwa ufeministi wa kibeberu nchini humo, soma mwanzo mpaka mwisho mwa riwaya hii ya kibabe. Furahia!
Publication Details
| Category | Riwaya |
| Publisher | TEPU |
| ISBN | 978-9-976-58401-1 |
| Date Published | 2025-06-19 |
| Publication Year | 2025 |
| Pages | 110 |
| Chapters | 9 |
| Language | Swahili |
| Academic | No |
| Visibility | Public |
| Formats |
Reading Access
Purchase or subscribe to unlock this content.
Open Reader